Psalms 57

Kuomba Msaada

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu! Utenzi Wa Daudi. Baada Ya Kumponyoka Sauli Pangoni)


1 aUnihurumie, Ee Mungu, unihurumie,
kwa maana nafsi yangu inakukimbilia.
Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia
mpaka maafa yapite.


2 bNamlilia Mungu Aliye Juu Sana,
Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.

3 cHutumana kutoka mbinguni na kuniokoa,
akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali;
Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.


4 dNiko katikati ya simba,
nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu:
watu ambao meno yao ni mikuki na mishale,
ambao ndimi zao ni panga kali.


5 eEe Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
utukufu wako na uenee duniani kote.


6 fWaliitegea miguu yangu nyavu,
nikainamishwa chini na dhiki.
Wamechimba shimo katika njia yangu,
lakini wametumbukia humo wao wenyewe.


7 gEe Mungu, moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

8 hAmka, nafsi yangu!
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.


9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;
nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

10 iKwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,
uaminifu wako unazifikia anga.


11 jEe Mungu, utukuzwe juu mbinguni,
utukufu wako na uwe duniani pote.
Copyright information for SwhKC